Posts

Showing posts from May, 2021

NI RAHISI KUJENGA DHAMANA YA UPENDO KWA MWANAMKE ALIYE HURU MOYONI KULIKO ALIYE FUNGWA NA MAUMIVU.

Image
Ifahamike kwamba MAPOKEO YA UPENDO HUZALIWA NA MOYO na huko ndiko chemi chemi za FURAHA NA AMANI hububujika Mwanamke ndiye MTUNZAJI NA MLEZI WA MAPENZI na kwa tafsiri hiyo ili Mwanaume awe katika MAHUSIANO AMA NDOA imara anawajibika kumpata MWANAMKE ALIYE HURU MOYONI Mwanamke hawi mwongozaji wa UPENDO katika mahusiano na ndoa ikiwa mwanaume hayupo katika UHALISIA "pure" kwa sababu Mwanamke anakuwa kwenye PENZI kwa kufuata moyo wake, ila tu anaishi kwa kufuata uwajibikaji wa Mwanaume katika penzi lao, Mwanaume kama hujawa tayari kuwa na Mwanamke kwa malengo ya UHUSIANO ENDELEVU usijaribu kumfanya Mwanamke awekeze UPENDO WAKE KWAKO Ni hasara kwa Mwanaume kumfanya Mwanamke ampende halafu yeye yupo kwa mtazamo wa HAJA YA MWILI Kuna wakati Mwanamke ataamua kuondoka nawe utakuwa umemzoea ndipo utaamini kwamba;- HATA PAKA NYUMBANI AKIPOTEA UTAM-MISS JAPO ALIKUWA HAKAMATI PANYA Mazoea yana taabu wahenga walisema, hivyo usimdharau Mwanamke kwa kujua HANA UJANJA KWAKO kisa uliisha m...

KOSA LA MWANAUME KATIKA MTAZAMO WAKE KWA MWANAMKE NI PALE ANAPOKUWA AMEKWISHA KUWA NAE

Image
Wanaume wengi kabla hajamjua MWANAMKE huwa na mtazamo wa THAMANI YA MWANAMKE na pindi wanapopata nafasi ya kuwa na mwanamke huwa na mtazamo wa kawaida juu ya MWANANKE Hilo ndilo huwafanya wanaume wengi kuona mwanamke ni kama chombo cha;- KULEA WATOTO. NGONO. UPISHI. MAANDALIZI YA UVAAJI NA USAFI. Na mengine yanayotokana na Mwanaume Kuhudumiwa, kwamba kama Mwanamke sio mchapa kazi anakosa sifa ya kuwa nae, na wanaume wengi wa aina hiyo Hafanyi chochote Mwanamke akiwepo Lakini kama MWANAUME angebakia na ule mtazamo wa awali kwa kujua THAMANI YA MWANAMKE naamini pasingekuwa na MWANAMKE ambaye angelilia MAPENZI na zaidi sana USALITI UNGEBAKIA KWA WENYE HULKA YA NGONO. Utu wa MWANAMKE upo katika maungo yake, kuamini kwamba;- ANAPO MVULIA NGUO MWANAUME HAPO NDIPO ANAKUWA AMEKABIDHI UTU WAKE KWA MWANAUME HUSIKA. Na inapokuwa tofauti Mwanamke huyo hujihisi kufanyiwa ukatiri, japo ni ukweli kuwa STAREHE YA MAPENZI NAYO HAIJAWAHI MWACHA MTHITAJI SALAMA Muda mwingine kinachopunguza hasira ya...

KWA DUNIA TULIYOPO HAKUNA HAKIKA YA MTU KUWA NA MTU AMBAYE NDO KWANZA YEYE YUPO PEKE YAKE

Image
Unaweza kujiuliza maswali mengi katika hili, lakini fahamu jambo moja;- MAPENZI IMANI. Ili mapenzi yakose maana ni pindi IMANI inapokuwa imetoweka, kila mtu awe mwanamke ama mwanaume anahitaji kuwa na UHUSIANO IMARA Lakini lipo tatizo wengi hatujalijua, nalo ni;- KUAMINISHWA UPO PEKE YAKO. Bila kujua kwamba MAPENZI MENGI YANAJENGWA KWA FARAJA ZAIDI YA UHALISIA Kwamba mtu anatoka alikotoka huku akiwa amejawa MAUMIVU baada ya kile alitarajia kukosekana, na anakuambia kuwa na UPENDO WA DHATI JUU YAKO huku ndani ya moyo wake bado kabeba mtu mwingine japo akitesekea FARAJA kwako. Unataka kujua kwamba HAKUNA MTU AMBAYE NI SPECIAL zaidi kinacho yabeba mapenzi ni imani, fahamu hili;- KILA UNAYE KUTANA NAE UJUE KAACHWA NA MTU. KUNA MTU ANATOKA NA ULIYEMUACHA. ULIYEMUACHA ANAPATA ALIYEACHWA. Sasa nafikiri umepata maana yangu na itakusaidia kutafuta wako mmoja na mkapendana na kujenga DHAMANA YA UPENDO ambao utawapeleka mbali, bila kuangalia KATOKA WAPI NA YEYE KUTOANGALIA UMETOKA WAPI Mapen...

KILICHO ONDOA FURAHA NA AMANI ITOKANAYO NA MAPENZI NI VIPANDE VYA KUJAZIA MAPENZI

Image
Kuna mgawanyiko wa vipande vya MAHUSIANO NA NDOA kukosekana kwa mtu uliye nae, na katika kuhangaika kutafuta kipande cha kujazia kwa kilicho meguka kwenye mtazamo wako kwa mwenza wako, ghafla anatokea mtu wa kujazia kipande ulichokuwa unakihitaji ndipo unapoweka rehani MAHUSIANO AMA NDOA YAKO Maana kumpata wa HITAJI LAKO KWA UKAMILIFU nae akakuchukulia wewe ni wake wa chaguo lake ni zaidi ya bahati, shida kwa mtu huyo:- JE KWELI ANAKUPENDA? Mara nyingi wa FULL PACKAGE KWAKO YEYE HAKUONI KAMA WEWE NI WAKE WA CHAGUO LAKE. Hapa ndipo utajua HUJUI MAANA YA MAPENZI Kuwa na mtu ambaye umeweza kuendana nae na wewe kukubari kwamba utamtengeneza kwa kubadili choice yako kwake ndipo utaweza KUPATA UPENDO WA DHATI kuliko kama ungefuata kuwa na mtu ambaye amekamilika vigezo vyako ila yeye hana UPENDO nawe, mara yingi TABIA HALISI ndizo zinatuingiza kwenye CHOICE ngumu Huwezi kutaka kupata HURUMA YA MTU WAKO ikiwa hujui kama huyo mtu wako anayo HURUMA JUU YAKO maana katika hilo ni wewe kuona uliy...

MWANAMKE USIFURAHIE KUTONGOZWA UKAJIONA UNAPENDWA BALI FURAHIA KUWA TAYARI UNAE UMPENDAYE

Image
Kuna faida kubwa kwa Mtu kuwa na mtu UMPENDAYE kuliko kuwa na mtu AKUPENDAYE ila wewe humpendi kwa sababu furaha na amani halisi inaanza na UTASHI wako mwenyewe Wengi tunajikuta njia panda kwa sababu ya kutaka kujua UPENDO WA MWINGINE KWAKO huku ukisahau kwamba:- UNAWEZA KUPENDWA NA MTU KWA SABABU ZAKE NA USIJUE JAPO KUNA UNAYO FURAHIA UKIAMINI NI UPENDO . Utashi ni mapokeo ya MOYO baada ya uhitaji wa NAFSI na hapo ndipo UPENDO hujengwa, ndo Maana hata ninasema ANZA WEWE KUPENDA Kabla ya KUPENDWA kwani Kuna faida, Maana ukimpenda mtu tafuta KUAMINIWA KATIKA UPENDO Ndipo utaona MAPENZI YANAVYO WEZA KUJITENGENEZA MENYEWE japo ni jambo linalohitaji Muda mpaka kufikia FURAHA NA AMANI YAKO Uwiano wa UPENDO haujawahi onekana, Ila kilicho kuwepo katika MAPENZI ni kukubari kwamba NAWEZA KUJENGA IMANI YA MWINGINE KUONA NAMPENDA ndipo iwe rahisi wewe kupendwa, Mfano hai :- MWANAMKE ANAWEZA KUWA NA MAWASILIANO NA MWANAUME ILA YEYE KAMA YEYE HAJAJENGA WAZO LA MAPENZI ILA MWANAUME ALIOMBA MAWASI...