USISHIRIKI MAHUSIANO NA MWANAMKE AMBAYE HAMHESHIMU MKEO 💯
Mtume Paulo alipata kusema:-
Kumekuwa na tabia mbaya miongoni mwa wanaume wengi, kukandamiza heshima za wake zao kwa Kujaribu kuhesabu madhaifu ya wake zao kiasi kwamba wanahisi Mwanamke huyo hafai kuwa Mke
Udhaifu wa kuhisi madhaifu ya mwingine ni moja ya kukosa kuijua THAMANI ya Mtu mwenyewe na hilo hupelekea kuona NJE YA NDOA KUNA MWANAMKE WA THAMANI ZAIDI KULIKO MKE HALALI kitu ambacho kinadhoofisha Sana MAANA YA NDOA
Namsoma ELIKANA na Mke wake HANNAH baada ya teso la kupata Mtoto hatimaye Hannah anapata huruma kwa Mumewe juu ya haja yake kuwa na Mtoto, hasa kwakuwa alipata ujumbe wa MUNGU kwamba katika uzao wake atapatika Mtoto ambaye atakuwa NABII WA MUNGU
Ukisoma kitabu cha kwanza cha SAMWELI unajua kwamba :-
Baraka ya Elikana iliwekwa katika umoja wake na Hannah, Japo Hannah alichelewa kuzaa mpaka akaruhusu Elikana azae na mjakazi wao PENINA lakini Mtoto wa agano alitakiwa azaliwe na HANNAH 
Tusiwadharau wanawake kwa sababu zinazotokana na Maisha tunayohitaji, iwe kizazi, mali, hata Mapenzi kwa UJUMLA wake, Hakuna Mwanamke special, Ila ni namna wewe Mwanaume unavyoweza kumfanya MKEO awe kama sio kufanana na Mwanamke uliyekuwa una wish uwe nae, Mwanamke ni taasisi inayojitegemea huwezi kuwa na wanawake zaidi ya mmoja ukaona THAMANI yao, Bali kuwa na Mwanamke mmoja ndipo thamani yake utaiona

Comments
Post a Comment